takeer.com

Takeer

Play
Mute
takeer.com
@malkia_quality_products
Hii video ni kwa wote wanaosema wanatukubali mm na mume wangu Mr Kisanga hi video ni miaka ya nyuma baada yakutoka kwenye harusi yetu hakika haikuwa rahisi ila kwa uweza wa Mungu bado tunaendelea vizuri na ndoa yetu ina amani,baraka na mafanikio tele…..bila Mungu hatuwezi lolote sisi ni wale tunaosaidiwa na Bwana.

Ni miaka kama 8 ss tangu tujuane nakuishi pamoja nimemjua kisanga nikiwa na miaka 23 jina la Bwana libarikiwe tunatazamia kuzeeka pamoja nampenda sana sana mume wangu na namshukuru Mungu kwa kunikutanisha nae…

Namuomba Mungu awape wenza waliosahihi wanawake wote na wanaume wote waliowema na wenye nia njema watu wakuishi nao nakudumu nakupendana wapate maendeleo na mafanikio kwenye maisha yao na shetani asipate nafasi kwenye umoja wao.

Lastly Mungu anakupa wakufanana nae hivyo basi angalia njia zako na matendo yako na ujue tu atakayekuja kwenye maisha yako ni vile ulivyo ww….jitahidi kuwa mtu mwema mwenye tabia nzuri zakumpendeza Mungu na wanadamu ili Mungu akupe wakuendana nae na aweze kukupa amani na sio kuwa mwiba wakukurudisha nyuma kimaendeleo.

Pia wakati unamtafuta mwenza mtangulize sana Mungu ili akupe chaguzi sahihi kama mm nilifunga tatu kavu bila kula wala kunywa chochote nikiwa kanisani tu siku zote hizo na baada ya huo mfungo mambo mengi kwenye maisha yangu yalibadilika ikiwemo matokeo ya chuoni nilifauli vzr mno mno tofauti na mwanzo na pia baada ya muda ndio nilipata maarifa yakuwa karibu na kisanga mpaka tumefika hapa leo….Mungu ndio kila kitu mambo mazuri makubwa mema yapo kwa Mungu mfalme mkuu mmiliki wa vyote hata kwa majaribu yako ukimuamini atakushindia.

Mungu wa mbinguni awape maarifa na hekima kama Suleimani na majibu ya maswali yenu…Mungu awakumbuke kwenye mnayoyafanya muwe washindi na awape nguvu yakusali nakumtafuta yeye siku zote nawapenda sana wateja wangu wapendwa Amen.
takeer.com
Play
takeer.com
takeer.com
takeer.com
Play
takeer.com
takeer.com
Play
takeer.com
Play